Samirah Yusuph
Busega.
Wazee mkoani Simiyu wameadhimisha siku ya wazee duniani wakikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa vitambulisho vya matibabu kwa wazee.

Siku ya wazee duniani katika Mkoa wa Simiyu imeadhimishwa ki mkoa wilayani Busega na kuhudhuriwa na mkuu wa Mkoa wa Simiyu David Kafulila ambapo wamebainisha kuwa upatikanaji wa huduma ya Afya kwa wazee bado ni changamoto.

Wamesema wakati huu ambao upatikanaji wa vitambulisho vya matibabu ukiwa ni wa shida bado kuna uhaba wa wataalamu wa afya ya wazee kwa ajili ya kuwahudumia, vifaa tiba, pamoja na madawa licha ya serikali kutenga fungu la asilimia sita kwa ajili ya wazee kwenye mfuko wa afya.

Akizungumza na wazee hao mkuu wa mkoa wa Simiyu David Kafulila ameahidi kusaidia ujenzi wa ofisi ya wazee Mkoa ili waweze kutambulika zaidi na kurahisisha upatikanaji wa taarifa zao.

Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Mkoa wa Simiyu unajumla ya wazee 68,175 sawa na asilimia 3.8 ya wakazi wa mkoa huo huku wazee 29,490 pekee tayari wamepata huduma ya kadi za matibabu kwa wazee.

Mwisho.