Jeshi la China lilirusha ndege zake 16 za kivita kwenye anga ya Kusini mwa Taiwan Jumapili, huku Marekani ikielezea wasiwasi wake juu ya hatua hiyo iliyoiita ya kichokozi kutoka China karibu na kisiwa kinachojitawala chenyewe ambacho China inadai kukimiliki. 

China ilituma ndege zake za kivita 38 katika eneo hilo siku ya Ijumaa na ndege 39 siku ya Jumaosi, idadi inayodaiwa kuwa ya juu tangu Taiwan ilipoanza kutoa ripoti ya ndege hizo kuruka katika anga yake mwezi Septemba mwaka 2020.

Taarifa kutoka wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani, kupitia msemaji wake Ned Price imeonya kuwa shughuli za china karibu na Taiwan zinatishia amani na uthabiti wa kanda nzima na kuiomba China kuacha kufanya hivyo mara moja. Price amesema Marekani itaendelea kuisaidia Taiwan kujilinda.