Mama mzazi wa Rapper Snoop Dogg aitwae Beverly Tate amefariki akiwa na umri wa miaka 70, chanzo cha kifo chake hakijatajwa lakini imeelezwa kwamba alilazwa Hospitali mwanzoni mwa mwaka huu.

Ni Mama ambae alimpenda Mungu na alikua karibu sana na kanisa na hata Snoop Dogg alilelewa kwenye mazingira ya kanisa alipokuwa mdogo.

Snoop aliwahi kusema Mama yake alikua muungwana na ndiye alimshawishi Snoop kumuomba msamaha Mtangazaji wa TV Gayle King aliyezungumzia kesi ya ubakaji ya Kobe Bryant wakati wa msiba wake mwaka 2020 kitendo kilichomkasirisha Snoop na kupost video akitumia lugha kali na kumkosoa”