Jeshi la Polisi linapenda kutangaza majina ya vijana wenye elimu ya shahada, stashahada, astashahada, kidato cha sita na kidato cha nne ambao walifanyiwa usaili na kuchaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi Tanzania kupitia Makao Makuu ya Polisi na Mikoani. 

Tarehe na utaratibu wa kuripoti Shule ya Polisi Moshi utatolewa na Makamanda wa Polisi wa Mikoa waliofanyia usaili na watatakiwa kwenda na nauli zao kulingana na mahali wanapotoka hadi Moshi.

Kwa vijana walioomba nafasi za ajira kupitia vikosi ambavyo vipo chini ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na kufanyiwa usaili Polisi Baracks Dar es Salaam, watatangaziwa siku ya kuripoti kupitia tovuti ya Polisi https://bit.ly/3pjUuLY.

Kwa mujibu wa kanuni za Shule ya Polisi Tanzania ni marufuku kufika shuleni na simu ya mkononi. Atakaepatikana na simu atafukuzwa mafunzo mara moja. Shule itaelekeza utaratibu wa kupata mawasiliano.

Orodha ya vijana waliochaguliwa kuhudhuria mafunzo ya awali ya kujiunga na Jeshi la Polisi nchini imeambatanishwa na tangazo hili.

👉Kuona majina ya waliochaguliwa kujiunga na jeshi la Polisi,BOFYA HAPA.

👉Kupata nafasi mbalimbali za kazi serikalini na makampuni binafsi,BOFYA HAPA