Maelfu ya wapoland walikusanyika kutetea uwanachama wa nchi yao katika Umoja wa Ulaya baada ya wiki iliyopita mahakama ya juu ya Poland kutangaza uamuzi wa kihistoria dhidi ya sheria ya mamlaka ya Umoja wa Ulaya.
Maandamano ya wanaounga mkono Umoja wa Ulaya yaliitishwa na aliyewahi kuwa mkuu wa Umoja wa umoja huo Donald Tusk ambaye sasa ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini humo ambaye ametahadharisha juu ya Poland kuondoka katika Umoja wa Ulaya.
Maelfu ya waandamanaji walijitokeza katika mji mkuu Warsaw na miji mingine zaidi ya 100 kote nchini Poland.
Tusk amewaambia wananchi kuitetea nchi yao ikiwa ndani ya Umoja wa Ulaya baada ya kushuhudiwa kauli za kuukosoa uamuzi wa mahakama yake ya juu uliotoka nje na kote katika nchi za Umoja waUlaya.