Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Arusha, Odira Amworo amesema kuwa ameridhika mashtaka dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake na kuwatia hatiani kosa unyang’anyi wa kutumia silaha .

Baada ya kuwatia hatiani wakili wa Serikali amesema hakuna kumbukumbu ya makosa ya zamani ya washtakiwa wote watatu, na kuiomba Mahakama iwape adhabu  ya miaka isiyopungiua 30 jela na viboko.