Kundi la watu wenye kujihami kwa silaha limewaua takribani watu 20, pale lilipolivamia eneo la soko moja huko katika jimbo la Sokoto nchini Nigeria. 

Taarifa ya mamlaka na bunge la nchi hiyo zimesema genge hilo la watu lilichoma moto pia magari. 

Mshauri maalumu wa waziri mwenye dhima na masuala ya kipolisi katika jimbo la Sokoto, Idriss Gobir alisema wahalifu hao walifyatula risasi mfululizo na kuwauwa watu kadhaa wakiwa kwenye pikipiki.

Tangu Desemaba mwaka jana eneo la Kaskazini magharibi mwa Nigeria kumeshuhudiwa wimbi la utekaji nyara kwa watoto wa shule na wanakijiji na watekaji kudani fedha ili kuwaachia mateka hao, hatua ambayo imevuruga maisha ya kila siku ya mamilioni ya watu.