Korea Kaskazini leo imefyatua kombora moja kuelekea pwani yake ya mashariki. 

Taarifa hizo zimethibitishwa na maafisa wa Korea Kusini na Japan, wakati Korea Kusini ikizindua maonyesho makubwa ya silaha.

 Hatua hii ni ya hivi karibuni kwa Korea Kaskazini kujaribu silaha zake na kuendeleza ajenda ya kuimarisha uwezo wake wa kijeshi, licha ya vikwazo vya kimataifa ilivyowekewa kutokana na programu yake ya silaha za nyuklia na makombora. 

Katika taarifa yake, Korea Kusini imesema inafuatilia kwa karibu hali na kuimarisha utayari wake kwa kushirikiana na Marekani, endapo kutakuwa na urushaji wa makombora mengine. 

Ufyatuaji huo umefanyika wakati wakuu wa intelijensia wa Marekani, Korea Kusini na Japan wakitarajiwa kukutana mjini Seoul kujadili mkwamo na Korea Kaskazini pamoja na masuala mengine.