Jaji mpya katika kesi ya uhujumu uchumi inayomhusisha Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu ni Joachim Tiganga.

Jaji Tiganga amejitambulisha katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi mbele ya washtakiwa na upande wa mashtaka

Kesi hiyo imepangwa kuendelea tena leo Jumanne Oktoba 26, 2021 baada ya kusimama kwa siku saba, tangu Oktoba 20, huku Jaji Kiongozi Mustapha Siyani aliyekuwa akiisikiliza alipojitoa kutokana na kuongezewa majukumu.