Jaji Mustapha Siyani ameanza kusoma uamuzi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Uamuzi huo umeanza kusomwa leo Jumatano Oktoba 20, 2021 saa 4: 00 asubuhi katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Jaji Siyani amesema ataanza kusoma kwa ufupi yale yaliyozungumzwa ambayo atayaona ni ya muhimu.

Kwa ujumla Jaji Siyani kwa Sasa anafanya rejea ya ushahidi wa upande wa mashtaka kwa muhtasari.