Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewataka askari wa Jeshi hilo kutimiza wajibu wao ili kuweza kukabiliana na matukio ya uhalifu na wahalifu pamoja na vitendo vingine vya uvunjifu wa amani vinavyojitokeza kwenye jamii.

IGP Sirro amesema hayo jana wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya Medani za kivita katika kambi ya Kambapori iliyopo West Kilimanjaro katika wilaya ya Siha ambapo askari wa kozi ya cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Polisi leo tarehe 08 Oktoba 2021 wanatarajia kuhitimu mafunzo yao ya miezi minne  na kupanda cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Polisi katika Shule ya Polisi Moshi.

 Naye Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Khamis Chilo amesema kuwa, Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ya kupandisha vyeo hasa kwenye Vyombo vya Ulinzi na Usalama ambapo Mheshimiwa Chilo pia amewataka askari Polisi kwenda kutimiza wajibu wao katika kuhakikisha usalama wa raia na mali zao.