Support ya Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kutoka kwa Wapiga kura wa Chama cha Republican imeendelea kuongezeka ambapo utafiti mpya wa uliofanyika kwa kura kupigwa umeonesha kwamba asilimia 78 ya Wanachama hao wa Republican wanataka kumuona Donald Trump akigombea tena kiti cha Urais katika uchaguzi wa mwaka 2024.

Asilimia hiyo 78 ni ongezeko la asilimia 12 kwenye kura kama hizo zilizopigwa mwezi May 2021 ambapo 66% ya Republican walisema wanataka arudi tena kugombea 2024 ambapo Chuo Kikuu cha Quinnipiac kimetangaza matokeo ya kura hizi mpya jana Jumanne ambazo zimepigwa kuanzia Oktoba 15 hadi 18 mwaka huu na kujumuisha Watu wazima 1,342 Nchi nzima.