Hukumu ya kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa Klabu ya Soka ya Simba, Evans Aveva na aliyekuwa makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ inatarajiwa kutolewa Oktoba 28, 2021 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka nane yakiweno ya kughushi, kujiapatia fedha na matumizi mabaya ya madaraka kwa kuhamisha fedha bila Kamati ya Utendaji ya Simba, kukaa kikao.

Awali, kesi hiyo ya jinai namba 214/2017 ilipangwa kutolewa hukumu jana, Oktoba 21, 2021, hata hivyo, imeahirishwa hadi wiki ijayo.

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba ambaye ndiyo anasikiliza shauri hilo, amesema bado hajamaliza kuandika hukumu. Hii ni mara ya pili katika mwezi huu kesi hiyo haitolewi hukumu.