Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Arusha, Odira Amworo amesema hakuna shaka washitakiwa watatu walifika dukani kwa Mohamed Saad siku ya tukio.

Pia, amesema amethibitisha mshitakiwa wa kwanza Lengai Ole Sabaya na mshitakiwa wa pili Sylivester Nyegu walikuwa wanafahamiana.

Hakimu Omworo amesema hayo leo Ijumaa Oktoba 15, 2021 wakati akiendelea kuchambua hoja wakati akisima hukumu ya Sabaya na washitakiwa wenzake watatu.

Akiendelea kuchambua hukumu hiyo, Hakimu Omworo amesema kuwa imethibitika mshitakiwa wa kwanza alikuwa na bastola ndani na nje kulikuwa na watu wawili wenye silaha hivyo, hakuna shaka duka la shahidi wa kwanza lilivamiwa na watu wenye silaha na lilikuwa chini ya watu wenye silaha.