Hivi karibuni kampuni ya Infinix imezindua Infinix zero x simu hii inakuja na sifa nzuri ambazo tumekuwa tukizisikia tangu kuzinduliwa kwake. Leo hii kupitia makala hii tutaenda kuangalia zaidi kuhusu mambo ya muhimu ya kwenye simu amabazo zitakupa sababu ya kuinunua.
 


Kamera Bora yenye uwezo wa kuzoom kwa umbali mrefu.

Moja kati ya sifa kubwa ya Infinix Zero X Pro ni pamoja na kamera, Simu hii kwa ujumla inakuja na kamera tatu kwa nyuma, huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 108 na nyingine mbili zikiwa na Megapixel 8 kila moja.
 

Kikubwa kuhusu kamera hizi ni uwezo wake wa kipekee wa kupiga picha ya kitu chochote kilichopo mbali. Hii inaonyeshwa kwa kuwa simu hii inaweza kupiga picha mwezi ambao umbali wake kutoka duniani ni takribani mile 238,855 kwa mujibu wa NASA. Kupitia kamera ya Infinix Zero X Pro utaweza kufanya uweze kuona mwezi upo karibu kabisa kupitia simu yako.
 

Hayo yote yana wezeshwa na teknolojia mpya Moonshot pamoja na lensi mpya ya 60x periscope telephoto, ambayo inaweza kuchukua picha au video na kuzoom hadi 5x.
 


Kioo Bora aina ya AMOLED

Kwa sasa Infinix Zero X Pro ni moja ya simu ambayo inakuja na kioo cha AMOLED, kioo hichi kinafanya uweze kuangalia video na picha zikiwa kwenye rangi bora na muonekano mzuri. Tofauti kabisa na vioo vilivyo tengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD.
 

Kioo cha Infinix Zero X Pro kinakuja na ukubwa wa inch 6.67 huku ikiwa na uwezo wa kuonyesha rangi zaidi ya Milioni 16 hii inafanya simu hii kuwa bora sana kwa Media za aina yoyote, kama wewe ni mpenzi wa kuangalia video na kucheza game kwenye simu basi simu hii utaipenda sana.


Sifa Bora za Ndani

Infinix Zero X Pro ni bora sio kwa muonekano tu, sifa za ndani za simu hii pia ni bora. Simu hii inakuja na processor yenye chipset yenye nguvu ya Mediatek Helio G95, processor hii ni bora sana kwa wale watumiaji wa nguvu wa simu ikiwa pamoja na kufanya kazi nyingi kwa pamoja ikiwa pamoja na kucheza game.
 

RAM ya GB 8 inaweza kusaidia kufanya chochote kwa haraka hii ikiwa pamoja na Virtual RAM ya GB 3 ambazo zote kwa pamoja zina uwezo wa kufungua programu nyingi kwa pamoja bila simu ku-kwama kwama.
 

Kwa upande wa uhifadhi wa ndani (ROM) simu hii imejitosheleza kwani GB 128 zitakusaidia kuhifadhi zaidi ya picha 18,800 za JPG zenye MB 7 kila moja, na GB 256 utaweza kuhifadhi picha zaidi ya 37,600 za JPG zenye MB 7 kila moja.
 


Kama hiyo haitoshi, Infinix Zero X Pro inakuja na sehemu ya memory card ambayo unaweza kuweka Memory card yenye uwezo wa hadi GB 512.
 

Uwezo Bora wa Kujaa Chaji Haraka
Katika ulimwengu wa sasa ambao kila mtu hana muda wa kutosha, ni wazi kuwa unahitaji simu ambayo ina uwezo wa kujaa chaji kwa haraka.
 

Infinix Zero X Pro inakuja na teknolojia ya Fast charging yenye uwezo wa kufanya battery ya simu hii ya 4500 mAh kujaa chaji kwa haraka takribani asilimia 40 kwa dakika 15 tu.
 

Hii inasaidia sana hasa pale unapotaka kutumia simu yako kwa haraka bila kuwa na muda mwingi wa kusubiri simu ijae chaji. Ukiwa na infinix Zero X Pro huna haja ya kuchaji simu yako usiku kucha.
 

Muundo Bora
 
Tukianza na muudo, simu hii imetengenezwa kwa muundo ambao ni tofauti na simu zote za Infinix Zero, muonekano wa Infinix Zero X Pro ni Glass mbele na nyuma, glass ya nyuma imetengenezwa kwa muundo mpya ambao imewekewa urembo ambao huwezi kuona kwenye simu nyingi za sasa.
 

Kwa pembeni simu hii inakuja na frame ya plastic. Hii inafanya simu nzima ya Infinix Zero X pro kuwa na uzito wa hadi gram 193 g ambayo ni sawa na kilogram 0.193 kg. Kifupi ni kuwa simu hii inamuonekano mzuri sana na ina feel vizuri sana ikiwa mkononi.

Hitimisho
Kwa ufupi kabisa hayo ndio mambo ya muhimu ambayo unatakiwa kuangalia kwenye simu ya Infinix Zero X Pro, kumbuka yapo mambo mengi sana kwenye mfumo wa Android 11 ambayo utayapenda kwenye simu hii.
 

Kwa sasa simu hii inapatikana hapa Tanzania kupitia maduka mbalimbali ya Infinix na pia kupitia maduka ya Tigo nchini kote, kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Infinix kupitia namba za simu +255744606222