Staa wa Ureno Cristiano Ronaldo leo ameandika rekodi mpya ya kuwa Mchezaji mwenye hat-trick nyingi zaidi duniani (10) kwa upande wa Timu za Taifa.

Ronaldo amefunga hat-trick yake ya 10 akiichezea Ureno katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Luxembourg katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.

Hadi sasa katika maisha yake ya soka Ronaldo amefunga jumla ya hat-trick 58 (Man United 1, Real Madrid 44, Juventus 3 na Ureno 10)