Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anakaribisha maombi ya kazi  kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi mia mbili thelathini na  tatu (233) kama zilivyoainishwa katika tangazo hili;
 

1.MHANDISI II UJENZI (HIGHWAY) – NAFASI 07 .

 SIFA ZA MWOMBAJI  
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne/Sita waliofuzu Mafunzo ya Shahada/  Stashahada ya Juu katika fani ya Uhandisi Ujenzi walioojiimarisha katika Ujenzi wa  Barabara (Bachelor of Science in Civil Engeneering – Highway) kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

2.MHANDISI II UJENZI (STRUCTURAL) - NAFASI 134 .

 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne/Sita waliofuzu mafunzo ya Shahada/  Stashahada ya Juu katika fani ya Uhandisi Ujenzi waliojiimarisha katika Miundombinu na Uimara wa Majengo (Bachelor of Science in Civil Engeneering - Structural) kutoka  
katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

3.MHANDISI II (UMEME) - NAFASI 09 .

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne/sita waliofuzu Mafunzo ya Shahada/  Stashahada ya Juu katika fani ya Uhandisi Umeme (Bachelor of Science in Electrical  Engeneering) kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

4. MHANDISI II UJENZI (BUILDING) - NAFASI 83

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne/sita waliofuzu Mafunzo ya Shahada/   Stashahada ya Juu katika fani ya Uhandisi Ujenzi waliojiimarisha katika ujenzi wa  Majengo (Bachelor of Science in Civil Engeneering - Building) kutoka katika vyuo   vinavyotambuliwa na Serikali.

 👉Kujua zaidi pamoja na kutuma Maombi <<BOFYA HAPA>>

👉Kupata nafasi mbalimbali za kazi Serikalini na mashirika binafsi <<BOFYA HAPA>>