Mohamed Said Issa (ACT Wazalendo), ametangazwa mshindi katika uchaguzi mdogo wa Jimbo Konde kwa kupata kura 2391

Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo Abdallah Said Ahmed amemtangaza Jumamosi Oktoba 9, 2021 katika kituo cha majumuisho cha Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Katika matokeo hayo, Issa amefuatiwa na mgombea wa CCM, Mbarouk Amour Habib aliyepata kura 794 kati ya kura 3,338 zilizopigwa.

Mgombea mwingine katika uchaguzi huo Salama Khamis Omar wa CUF alipata kura 98 na Hamad Khamis Mbarouk (AAFP) akipata kura 55.