Watanzania Tunaweza Tuwekeze Kwenye Uchimbaji Mkubwa Wa Madini- Prof Manya
Wizara ya Madini imeipongeza kampuni ya kitanzania ya Javan Investiment and Co Ltd kwa kutumia utaalamu waliosomea nchini kuwekeza katika utafutaji wa madini ya Almasi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Madini Mhe.Prof.Shukrani Manya wakati alipotembelea kampuni iyo kukagua maendeleo ya mradi huo katika eneo la mberekese,Iramba.
“Siku zote tumekuwa tukiamini kwamba uwekezaji mkubwa wa utafutaji madini nchini lazima uhusishe kampuni za kigeni,lakini hawa wanatoa mfano hai wa namna ambavyo mtanzania anaweza akasoma na kuweka uzoefu wake wa kufanya kazi katika kampuni tofauti na akaanzisha kampuni yake ya uwekezaji katika shughuli za madini na matokeo yake ndo tunayaona hapa”, amesema.
Ameongeza kuwa kuanzishwa kwa mgodi huo nchini utakuwa ni mgodi mwingine mkubwa wa kitanzania ambao utazalisha almasi kwa wingi.
Ametoa rai kwa watanzania kuthubutu kufanya shughuli ambazo zinausisha uwekezaji mkubwa kwani uwezo wanao
Aidha amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Iramba kushirikiana na Ofisi ya Afisa Madini mkazi ili kushughulikia migogoro ya uchimbaji wa madini kwani litasaidia kutatua migogoro iyo kwa haraka ili kazi za uchimbani wa madini ziendele na mapato yapatikane.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iramba,Suleiman Mwenda amesema wamefarijika na ugeni huo na lengo lao kubwa kwa sasa kama wilaya ni kuongeza uzalishaji wa madini ambapo kwa msimu uliopita walizalisha gramu 317000 na kuingiza bilioni 36 kutoka katika madini ya dhahabu kwa ujumla.
“Kwa sasa tuko katika kuongeza wigo wa wawekezaji zaidi wa madini kwani tuna maeneo mengi yenye dhahabu katika Wilaya yetu ili tuongeze uzalishaji na tuna watu zaidi ya elfu kumi ambao wamejiajiri kwenye uchimbaji na pia kwa sasa tunakusanya mapato yetu katika eneo hilo maana utachangia katika ucumi wetu kwa ujumla”,ameongeza.
Naye mwekezaji wa Mgodi huo Bw.Javan Bidogo amesema wameshukuru kwa ujio wa Naibu Waziri uyo kwani umewatia nguvu kuona Serikali iko karibu nao na inawapa ushirikiano wa kutosha,amesema mgodi huo mpaka sasa umeajiri wafanyakazi 50 katika kipindi hiki cha utafiti lakini wakifikia kipindi cha uzalishaji wataajiri wafanyakazi 1000 patika kila mgodi watakaokuwaa wameanzisha.
kwa sasa nchini migodi mikubwa ya Almasi inahusisha mgodi wa mwadui ambao upo tangu miaka 1940 na mingine ni midogo sana.