Maofisa wanne wa jeshi la Rwanda wameuawa nchini Msumbiji, katika operesheni ya kijeshi dhidi ya wanamgambo wa kiislamu, katika jimbo la Cabo Delgado.

Taarifa kutoka nchini Rwanda zinasema, wanajeshi wengine 14, wamejeruhiwa vibaya katika mapigano hayo.
 

Hii ni mara ya kwanza kwa Rwanda kutangaza majeruhi katika kikosi chake cha wanajeshi 1,000 kilichopo nchini Msumbiji, tangu waanze operesheni ya kukabiliana na wanamgambo hao.

Haijawekwa wazi ni katika eneo gani haswa la jimbo la Cabo Delgado, ambako wanajeshi wa Rwanda waliuawa.

Jumamosi iliyopita, marais wa Msumbiji – Filipe Nyusi na wa Rwanda, Paul Kageme – waliwapongeza wanajeshi ambao wamejitoa kupambaa na magaidi.

Rwanda imepeleka nchini humo wanajeshi 1,000 kukabiliana na wapiganaji hao wanafanya mashambulizi ya uharibifu kaskazini mwa taifa hilo.