Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel.

Katika mazungumzo hayo, Merkel amempongeza Rais Samia kwa kushika hatamu za Urais nchini Tanzania na kumpa pole kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya tano, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli. Pia amempongeza Rais Samia kwa jitihada zake za kupambana na UVIKO 19 na kuahidi kuunga mkono jitahada hizo kwa kutoa msaada wa chanjo za kukabiliana na ugonjwa huo.

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel.

Katika mazungumzo hayo, Merkel amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kushika hatamu za Urais nchini Tanzania na kumpa pole kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya tano, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli. Pia amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kupambana na UVIKO 19 na kuahidi kuunga mkono jitahada hizo kwa kutoa msaada wa chanjo za kukabiliana na ugonjwa huo.

Aidha, Merkel amesema mwezi Oktoba mwaka huu Serikali yake itaanzisha majadiliano na Serikali ya Tanzania kuhusu maeneo ambayo Serikali ya Shirikisho la Ujerumani inaweza kusaidia kutokana na athari za UVIKO 19.

Pia, Merkel amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini ambapo ameahidi kuwashawishi wafanyabiashara wa Ujerumani na watalii kutembelea na kuwekeza nchini Tanzania.

Kwa upande wake Rais Samia Suluhu Hassan amemshukuru Merkel kwa ushirikiano wake na Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo. Amempongeza kwa kumaliza kipindi chake cha uongozi akiwa ni kiongozi wa kisiasa mwanamke aliyeongoza muda mrefu ndani ya Chama chake cha CDU na ndani ya Jumuiya ya Ulaya.

Aidha, Merkel amesema mwezi Oktoba mwaka huu Serikali yake itaanzisha majadiliano na Serikali ya Tanzania kuhusu maeneo ambayo Serikali ya Shirikisho la Ujerumani inaweza kusaidia kutokana na athari za UVIKO 19.

Pia, Merkel amempongeza Rais Samia kwa jitihada zake za kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini ambapo ameahidi kuwashawishi wafanyabiashara wa Ujerumani na watalii kutembelea na kuwekeza nchini Tanzania.

Kwa upande wake Rais Samia amemshukuru Merkel kwa ushirikiano wake na Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo. Amempongeza kwa kumaliza kipindi chake cha uongozi akiwa ni kiongozi wa kisiasa mwanamke aliyeongoza muda mrefu ndani ya Chama chake cha CDU na ndani ya Jumuiya ya Ulaya.