Serikali ya Uingereza imetangaza kuwaweka tayari madereva wa kijeshi ili kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya mafuta ya petroli. 

Uingereza inakabiliwa na uhaba wa madereva wa malori baada ya kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya. 

Nchi hiyo imetangaza kuwa madereva wa malori ya jeshi watakuwa tayari kusambaza mafuta pale inapohitajika. 

Waziri wa Biashara wa Uingereza, Kwasi Kwarteng amesema nchi hiyo bado ina akiba ya kutosha ya mafuta na usambazaji bado ni mkubwa. 

Hata hivyo, Kwarteng amesema wanafahamu kuhusu masuala ya ugavi katika vituo vya mafuta na wanachakua hatua kukabiliana na tatizo hilo kama kipaumbele chao.