Uganda imetangaza kuwa, inakusudia kuwapatia chanjo ya Covid-19 watu wasiopungua milioni sita ifikapo mwisho wa mwaka, kabla ya shule kufunguliwa.

Karibu watu milioni 4.8 ya hao wameorodheshwa kama kipaumbele cha juu, ambapo ni pamoja na wafanyakazi wa sekta ya afya, walimu, wanafunzi wenye umri wa miaka 18 na zaidi, na wafanyakazi wa usalama.

Sekta ya elimu itafunguliwa tena mnamo Januari 2022, isipokuwa vyuo vikuu na taasisi zingine za elimu ya juu, ambazo zitafunguliwa kuanzia Novemba Mosi mwaka huu.

Wakati huo huo, Rais Yoweri Museveni ametoa agizo la kufunguliwa Misikiti na makanisa kwa ajili ya waumini kufanya ibada huku maeneo ya starehe kama baa na kwingineko yakiendelea kufungwa. Hata hivyo agizo hilo linaweka sharti la kutozidi watu 200 katika eneo moja la kufanya ibada sambamba na kulindwa miongozo ya afya ya kujikinga na viirusi vya corona