Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anatangaza nafasi za ajira 350 za cheo cha Konstebo wa Uhamiaji kwa vijana waliofuzu Mafunzo mbalimbali ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) au Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) waliopo Makambini au waliohitimu mafunzo hayo na wenye sifa zifuatazo :-
  1. Awe raia wa Tanzania mwenye umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 25.
  2. Awe na Cheti cha Kuzaliwa (Birth Cetificate} ,
  3. Awe na Namba au Kitambulisho cha Taifa (NIDA).
  4. Awe amehitimu Kidato cha Nne na ufaulu wa Daraja la Nne kwa Alama 28 hadi 31.
  5. Awe na Vyeti vya kuhitimu shule (Leaving Certificates),
  6. Awe Vyeti vya taaluma (Academic Certificate),
  7. Awe na Cheti cha Kuhitimu Mafunzo ya Awali ya JKT/JKU katika Oparesheni Mbalimbali.
  8. Awe na afya njema ya mwili na akili, na aambatishe Taarifa ya Daktari kutoka katika Hospitali yoyote ya Serikali.
  9. Awe na tabia njema, asiwe amewahi kufungwa, au kujihusisha na matumizi au biashara ya dawa za kulevya, au uhalifu wa aina yoyote.
  10. Asiwe na alama yoyote au michoro katika mwili wake.
  11. Asiwe ameoa au kuolewa.
  12. Asiwe ameajiriwa/hajawahi kuajiriwa Serikalini.
  13. Awe tayari kuhudhuria Mafunzo ya awali ya Uhamiaji. 
  14. Awe tayari kufanya kazi mahali popote nchini Tanzania.


==>>Kujua Zaidi pamoja na Kutuma Maombi,BOFA HAPA 

Mwisho wa Maombi: 13.10.2021 


==>>Kujua Zaidi pamoja na Kutuma Maombi,BOFA HAPA 
Mwisho wa Maombi: 13.10.2021