Spika wa Bunge Job Ndugai, ameomba radhi kwa waumini wa dini ya Kikristo na Watanzania wote waliokwazika na kauli yake aliyoitoa jana Bungeni jijini Dodoma akielezea mstari wa Biblia.

Taarifa ya iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kitengo cha mawasiliano na uhusiano wa Kimataifa Ofisi ya Bunge imeeleza kuwa, Spika Ndugai alikusudia kuelezea Yusufu alitembea na mke wake kutoka Nazareti kwenda mpaka Yerusalemu kuhesabiwa na si Yesu kama alivyotamka