Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amemuapisha Dkt. Stergomena Lawrence Tax kuwa Mbunge wa Bunge hilo.

Dkt. Tax ameteuliwa mapema hii leo na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mbunge kutoka kwenye nafasi kumi za Wabunge wa kuteuliwa na Rais.

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Tax alikuwa Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ambaye amemaliza muda wake mwezi Agosti mwaka huu.

Akizungumza baada ya kumuapisha, Ndugai amesema amefanya hivyo mara baada ya kupokea taarifa ya uteuzi kutoka kwa Rais Samia.

Amempongeza kwa kazi kubwa ya kuwa Katibu Mtendaji SADC,”nasikia fahari kubwa kuwa miongoni mwetu karibu nyumbani,”amesema.