Shahidi wa pili katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu , Mkaguzi wa Jeshi la Polisi Mahita Mahita, amemaliza kutoa ushahidi wake.
 

Mahita aliyekuwa Msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha, amemamliza kutoa ushahidi huo leo Jumatatu, tarehe 20 Septemba 2021, mahakamani hapo mbele ya Jaji Mustapha Siyani.

Shauri hilo dogo lilitokana na mapinganizi ya mawakili wa utetezi, wakiongozwa na Wakili Peter Kibatala, wakipinga maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa pili katika kesi ya msingi, Adam Kasekwa, yasitumike mahakamani hapo kama kielelezo na Kamanda Kingai, katika kesi ya msingi, wakidai yalichukuliwa nje ya muda kisheria.

Pia, katika mapingamizi hayo walihoji kwa nini mtuhumiwa alihojiwa Dar es Salaam, badala ya Moshi mkoani Kilimanjaro alikokamatwa.

Mbowe na mwenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka sita yakiwemo ya kula njama na kufadhili fedha kwa ajili ya vitendo vya kigaidi.