Serikali Kutumia Bilioni 75 Kukarabati Na Kuboresha Hospitali Kongwe
Na. Angela Msimbira KISARAWE
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali itazikarabati na kuziboresha Hospitali za Wilaya za zamani ili ziweze kufanana za Hospitali za Wilaya Mpya zinazoendelea kujengwa nchi nzima.
Ameyasema hayo leo wakati akikagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa Mkoani Pwani,
Waziri Ummy amesema Serikali itaanza kuzikarabati na kuziboresha Hospitali za Wilaya Kongwe 50 na kila Hospitali itapatiwa kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya kuboresha na kujenga majengo ya hospitali hizo
Amesema kuwa Serikali inategemea kutumia shilingi bilioni 75 kwa ajili ya kuboresha Hospitali Kongwe za Wilaya ili zifanane na hospitali mpya zilizojengwa nchi nzima