Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Yamungu Kayandabila kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC).
 
Dkt. Kayandabila ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
 
Rais Samia Suluhu Hassan pia amemteua Dkt. Naomi Katunzi kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kwa kipindi kingine cha miaka mitatu mitatu.
 
Uteuzi wa viongozi hao umeanza tarehe 14 mwezi huu.