Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi ameivunja bodi ya ushauri ya kudhibiti vileo Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Zena Said imesema hatua hiyo ni kuanzia  Jumanne Septemba 7, 2021.