Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis amekosoa kuhusika kwa nchi za Magharibi Afghanistan kama jaribio la kuilazimishia demokrasia nchi hiyo. 

Papa amezungumzia suala hilo kwa kutumia maneno ya Rais wa Urusi Vladimir Putin akifikiria kwamba anamnukuu Kansela wa Ujerumani Angela Merkel.

 Alipoulizwa swali kuhusiana na Afghanistan katika mahojiano na kituo kimoja cha redio mjini Marid, kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki amesema atajibu kwa nukuu ya Kansela wa Ujerumani ambaye anamchukulia kama "mmoja wa wanasiasa wakuu duniani" ingawa maneno aliyoyasema yalisemwa na Rais Putin mwezi uliopita mjini Moscow alipotembelewa na Kansela Merkel. 

Papa amesema ni kukosa kujukumika iwapo mtu ataswashurutisha wengine kufuata yale anayoyataka yeye bila kuzingatia tamaduni na dini yao.