Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amesema anayaombea mataifa mengi yaweze kuwahifadhi wakimbizi wa Afghanistan, akisisitiza ni muhimu kwa vijana wa Afghanistan kupata elimu. 

Kwenye hotuba yake ya kila wiki katika uwanja wa mtakatifu Petro, Papa amesema anayaombea mataifa hayo yawalinde wale wanaotafuta maisha mapya. 

Papa Francis yuko msitari wa mbele kutetea haki za wakimbizi na wahamiaji. Maelfu ya waafghanistan waliookolewa na Marekani wanasubiri katika kile kinachojulikana kama vituo vya muda ndani ya mataifa kama Qatar Ujerumani na Italia. 

Maelfu ya raia wengine wanajaribu kuitoroka nchi na kuingia taifa jirani la Pakistan. 

Mara ya mwisho kundi la Taliban lilipokuwa madarakani nchini Afghanistan, wanawake hawakuruhusiwa kufanya kazi na watoto wa kike kunyimwa nafasi ya kwenda shule.