Wanaume wengi wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo la kutokwa na vipele mara tu baada ya kunyoa ndevu zao.
                    
Mbaya zaidi asilimia kubwa ya wanaume wamekuwa wakishindwa kujua nini cha kufanya ili kuondoa tatizo hilo ambalo pia huharibu muonekanano wa mhusika.

Hapa napenda kukueleza kuwa tunda la parachichi nalo huweza kuondoa tatizo hilo au kupunguza madhara kwa mtu mwenye shida hiyo.

Jambo la kufanya ni kupata tunda hili fresh kisha limenye na baadaye kulisaga halafu utalitumia mara tu baada ya kunyoa ndevu zako kwa kupaka rojorojo hilo la parachichi sehemu zote za kidevu yaani hii unaweza kuiita 'after shave ya asili'.

Tunda hili la parachichi linauwezo wa kuondoa tatizo hilikutokana na kuwa mafuta mazuri kwa ngozi ambayo pia husaidia kufanya ngozi kuteleza na kuwa laini na yenye afya.