Watu wapatao 41 wamekufa baada ya moto kutokea katika gereza  la Indonesia lililopo pembezoni mwa mji mkuu wa Jakarta.

Moto huo ulitokea majira ya asubuhi sana siku ya Jumatano katika gereza la Tangerang wakati wafungwa wengi wakiwa wamelala.

Kulikuwa na wafungwa 122 katika gereza C ambalo liliathiriwa na moto.

Watu kadhaa wanadaiwa kujeruhiwa huku wengine wakiwa mahututi.

Hitilafu ya umeme inadaiwa kuwa chanzo cha moto huo.

-BBC