Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi, Joanfaith Kataraiya na dereva wake wamepata ajali baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kupasuka tairi ya mbele na kupinduka katika Kijiji cha Usangule wilayani Malinyi.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Mathayo Masele amesema ajali hiyo ilimetokea Septemba 05, mwaka huu majira ya saa moja kasoro jioni. Kwa saa za Afrika Mashariki.

Masele amesema walipata taarifa ya ajali hiyo kutoka kwa mkurugenzi mwenyewe baada ya kunusurika na walifika eneo la ajali kijiji cha Usangule kilometa 25 kabla ya kufika Malinyi.

Amesema licha ya maendeleo mazuri ya mkurugenzi huyo aliyejeruhiwa zaidi miguuni na dereva aliyelalamikia kuumia mgongo na kichwa, ajali hiyo ilikuwa ni mbaya kwa tairi kupasuka na gari kupinduka na tairi kuwa juu.

Hata hivyo amesema majeruhi hao wawili walihamishwa kutoka kituo cha afya Mtimbira majira ya saa tano usiku baada ya matibabu ya awali na kupelekwa hospitali ya Rufaa ya St Francis iliyopo Ifakara wilayani Kilombero kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kiafya na matibabu zaidi.