Kundi la Wanamgambo wa Taliban na vikosi vya wapiganaji pinzani wamekabiliana siku nzima ya Jumamosi kudhibiti jimbo la Panjshir kaskazini mwa mji wa Kabul, eneo la mwisho nchini Afghanistan kutoa upinzani mkali dhidi ya Taliban.

Pande zote mbili zimedai kuwa zinalidhibiti eneo la juu la bonde la Panjshir lakini hakuna upande wowote uliweza kutoa ushahidi wa hilo.

Msemaji wa Taliban Bilal Karimi amearifu kuwa wilaya za Khinj na Unabah zimekamatwa hatua iliyowezesha wapiganaji wa Taliban kuchukua udhibiti wa wilaya nne kati ya saba za jimbo la Panjshir.

Hata hivyo kundi la wapiganaji wa National Resistance Front of Afghanistan wanaomtii kiongozi wa eneo la Panjshir Ahmad Massoud limesema "mapambano makali" bado yanaendelea.