WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameiwakilisha vyema Tanzania alipohutubia Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Jijini New York, Marekani.

Amesema kuwa Rais Mheshimiwa Samia ametoa ujumbe maalum ambao Tanzania ulitaka Mataifa mengine yasikie na kuiunga mkono kwenye mipango yake ya maendeleo.

Mheshimiwa Majaliwa ametoa kauli hiyo jana (Ijumaa Septemba 24, 2021) baada ya kukagua maendeleo ya mradi mkubwa wa maji wa Mwanga-Same, Wilayani Mwanga, Kilimanjaro

Waziri Mkuu ameongeza kuwa hotuba hiyo pia imeyaonesha M mengine duniani kile Tanzania inakifanya kina lengo la kuwapelekea wananchi wake maendeleo. “Mheshimiwa Rais ametumia mkutano huo kutakaribisha Mataifa  rafiki yenye nia njema ya kuja Tanzania kuwekaza waje. Wito wake huo unamanufaa makubwa kwetu”.

Akizungumza kuhusu mradi wa Maji wa Mwanga-Same ambao utahudumia wananchi wapatao 438, 931, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Nishati kuhakikisha inatengeneza mfumo kwa haraka ili kusukukuma maji kutoka kwenye mashine na maji yaanze kusafirishwa”.

Pia Waziri Mkuu amemtaka mkandarasi anayejenga mradi huo kumaliza majadiliano na Wizara ya Maji na kukubaliana jambo la kufanya ili kuhakikisha wanaukamilisha mradi huo kwa muda uliopangwa na wananchi waanze kupata huduma ya maji.

Aliongeza kuwa, Rais Mheshimiwa Samia amedhamiria kuhakikisha kampeni yake ya kumtua mama ndoo kichwani inatekelezwa kwa vitendo. “Kampeni hii itawawezesha wananchi kupata maji kwa ukaribu.”

(mwisho)

 

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU