Zaidi ya maafisa 100 wa chama cha Tunisia cha Ennahda, ikiwa ni pamoja na wabunge na mawaziri wamejiuzulu kupinga utendaji wa uongozi wa chama chama hicho. 

Hatua hiyo ni pigo kubwa kwa chama hicho kilichogawanyika. Chama cha Ennahda, kikubwa bungeni, kimetumbukia kwenye mgogoro kutokana na jinsi kilivyoshughulikia hatua ya Rais Kais Saied kufuta kazi mawaziri wa serikali na kusimamisha bunge Julai 25, hatua ambayo upinzani iliilinganisha na mapinduzi ya kijeshi. 

Katika taarifa ya pamoja, maafisa hao 113 wamesema wamejiuzuli kazi kutokana na jinsi uongozi wa chama ulivyoshindwa kushughulikia maamuzi ya Saied.