WAZIRI MKUU wa Zamani, Edward Lowassa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa hotuba yake katika Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kusema kiongozi huyo amefanikiwa kulirejesha taifa katika ramani ya dunia.