Kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya ugaidi leo imeanza kusikilizwa mahakama kuu divisheni ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi.
Leo kesi hiyo inaendelea katika hatua ya usikilizwaji wa pingamizi la awali lililowekwa na washtakiwa kupitia kwa jopo la mawakili wao 14 wakiongozwa na Peter Kibatala.
Katika pingamizi hilo washtakiwa hao wanadai kuwa hati ya mashtaka ina kasoro za kisheria pamoja na mambo mengine wakidai kuwa sheria ya ugaidi ambayo wanashtakiwa nayo haijafafanua viambato vya kosa la ugaidi