Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imeanza kupokea ushahidi kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Ramadhani Kingai katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Kamanda wa polisi ni miongoni mwa mashahidi katika keshi hiyo, mashahidi wengine ni pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz.

Wengine ni maofisa wa polisi kutoka makao makuu ya jeshi hilo vitengo vya makosa ya kimtandao, uchunguzi wa silaha na uchunguzi wa maandishi na wengine kutoka mikoani.