Serikali ya Sudan imetangaza kuwa imetibua na kuzima jaribio la mapinduzi la kuiangusha serikali hiyo na kutoa mwito kwa wananchi kuwa watulivu sambamba na kuwahakikishia kuwa inadhibiti hali ya mambo.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, waliohusika katika jaribio hilo la mapinduzi walitaka kudhibiti kituo cha radio ya taifa hata hivyo hawakufaulu.

Vyombo vya habari vya serikali vimesema: "kulikuwa na jaribio la mapinduzi lililoshindwa, lazima watu wakabiliane nalo,".

Kwa mujibu wa duru hizo za habari waliopanga njama walijaribu kudhibiti jengo la shirika la utangazaji la serikali, lakini "hawakufaulu."

Msemaji wa serikali amesema zoezi la kuwahoji wanaoshukiwa kuhusika na jaribio hilo la mapinduzi litaanza muda mfupi ujao.