Jaji Elinaza Luvanda wa Mahakama Kuu Divisheni ya makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi aliyekutwa anasikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi namba 16/2021 yenye mashtaka sita yakiwemo ya Ugaidi, amejitoa kusikikiza kesi hiyo.
.
Sababu ya kujitoa katika kesi hiyo ni kutokana na mshtakiwa wa nne katika kesi hiyo, Mhe.Freeman Mbowe kuieleza mahakama hiyo kuwa yeye na washtakiwa wenzake watatu hawana imani na Jaji huyo na wana mashaka kama katika kuendesha kesi hiyo kama haki itatendeka.

Mbowe ametoa madai hayo leo Jumatatu Septemba 6, 2021 muda mfupi baada ya Jaji Luvanda kutupilia mbali mapingamizi mawili kati ya matatu yaliyowasilishwa mahakamani hapo dhidi ya washtakiwa hao.

Mbowe amedai kuwa wanavyoona mwenendo wa kesi yao hawatatendewa haki, hivyo wanaomba Jaji ajiondoe kusikiliza shauri hilo.