Infinix ZERO X pro:  simu pekee yenye uwezo wa kupiga picha ya mwezi angani kuzinduliwa.

Kupitia kurasa ya @infinixmobiletz kampuni ya simu Infinix imetangaza rasmi uzinduzi wa Infinix ZERO X pro simu ya kwanza kuja na camera ya MP108 na 60X periscope zoom lens.
 
 Infinix inatazamia kuzindua Infinix ZERO X pro 30/9/2021 kwa kushirikiana na Kampuni ya Tigo Tanzania. Infinix ZERO X pro ni simu ya kwanza kukidhi vigezo vya kupiga picha za ANGA hii imethibitishwa na Royal Observatory Greenwich ya jijini Londoni.
 
Baada ya tafiti mbalimbali kufanyika na Astronomers wataalamu wa ANGA ‘Royal Observatory Greenwich’ wamebaini kamera ya Infinix ZERO X pro ina injini ya Galileo Algorithm inayopatikana kwenye zoom lens 60x periscope inaongeza nuru (resolution) wakati wa uchukuaji picha ya Mwezi (moonshot camera) na hii kuifanya Infinix ZERO X pro kuwa simu ya kwanza kufaulu jaribio hilo.
 
Infinix ZERO X pro mbali ya kupata sifa nyingi mitandaoni baada ya uzinduzi wake wa mara ya kwanza kufanyika kupitia njia ya mtandao jijini londoni lakini Infinix imejizolea sifa kutokana na maboresho makubwa ya kioo kutoka kwenye IPS LCD na refresh rate ya 90HZ hadi AMOLED FHD+ na refresh rate ya 120HZ.
 
Kufahamu mengi zaidi kuhusu Infinix ZERO X pro tafadhali tembelea https://www.infinixmobility.com/