Hakuna mtu anaependezwa na mpenzi anaeboa. Na kwa mioyo ya kiume hakuna sehemu inayowauumiza na kuwaacha wamejawa maswali mengi na paniki kede kede kama pale mambo yanapokuwa hayaendi vizuri kitandani.

1.Unaomba ruhusa
Kama ukiwa unauhusiano wa muda mrefu na mwanamke na umeshaelewa lugha yake ya mwili na hisia zake, hakuna kinachomuondoa kwenye hali ya kihisia kama kuombwa ruhusa ya kiofisi kuendelea na jambo hasa juu ya yale mambo yetu mazuri, hauhitaji karatasi ya mahakama ya ruhusa kuendelea kumpa vishawishi na kumtekenya. 

2.Unatabirika
Kama mmekuwa pamoja kwa muda mrefu, hii ndio litakuwa tatizo kubwa maana sababu ya kwanini mara ya kwanza mapenzi yalikuwa matamu kitandani kati yako na yeye ni kwa sababu ulikua hujui nini cha kutarajia. Kama ukiwa unataka kurudisha khali kama awali inakupasa ubadilishe ratiba na ufanyaji wa mambo ili kuleta hali flani ya upya katika uhusiano wenu. Usiogope kujaribu vitu vipya. 

3.Mapenzi ya kukurupuka
Mwanamke wako sio punda wa kupandwa bila matayarisho, hajawa doli la kuchezea. Wanawake wote hupendwa kutayarishwa na kupewa mapenzi ya huba yenye hisia.

4.Haujiongezi inavyopaswa
Japo wanawake wengi huwa ni rahisi kukubaliana na staili ya mapenzi kutokana na wenza wao, ila iwapo kama unatumia staili hio hio kila mkikutana na hamna vionjo vyovyote vinavyobadilika lazima mwenza wako achoke na kuboleka na utendaji wako wa kazi. Kwahio kama ukitaka asikuchoke inabidi ujiungeze na ufanye mabadiliko ya hapa na pale.

5.Hautumii maneno au unayatumia kupitiliza
Kutumia sana maneno flani matata kumnongoneza masikioni humfanya mwanamke apandishe mrukhani kwa fujo, ila usitumie maneno yaleyale maana kurudia rudia maneno huyaondolea maana husika na kuyafanya butu. Jaribu kuyatumia katika wakati muafaka na mudi iliyosahihi na fanya uchaguzi mzuri wa maneno matamu yanayoongeza akshi za kimahaba.

6.Fanya majaribio
Kama upo na mwanamke kwa muda mrefu na unataka mambo chumbani yanoge, unapaswa kubadilisha mikao, jaribu mikao mingine ya kimapenzi, zungumzeni na mwambiane anapendelea nini na angependa kujaribu kipi, mawasiliano ni nguzo kubwa inayoweza kubadilisha mazingira na kufanya staili anayoitamani.

Kumbuka kinyume cha maboreko ni mafurahisho, ukitaka kufurahi jaribu kitu kipya ambacho hujawahi fanya au fanya unachokipenda ila kwa mguso tofauti na fikra mpya.