Baada ya ya Cristiano Ronaldo jana kufunga goli mbili kwenye mechi ya Portugal vs Ireland na kuifikia rekodi ya kuwa Mchezaji mwenye magoli mengi kwenye Timu ya Taifa, ameingizwa kwenye kitabu cha kumbukumbu za rekodi za dunia cha Guiness.

Ronaldo amempokonya rekodi hiyo Mchezaji wa Iran Ali Daei mwenye magoli 109 ambapo mpaka sasa Ronaldo ameichezea Ureno mechi 180 na Daei ameichezea Iran mechi149.