Bondia maarufu kutoka Ufilipino Manny Pacquiao ametangaza rasmi kuwa atagombea Urais wa Nchi hiyo kwenye Uchaguzi wa Mwakani huku akisema atahakikisha anatokomeza rushwa, umasikini na kuwa na Serikali yenye uwazi.
Pacquiao (42) ambaye ni Seneta nchini humo ametoa kauli hiyo baada ya kukubaliana na uteuzi wa yeye kuwania Urais uliofanywa na Chama chake cha PDP- Laban ambacho ni Chama tawala kilichomuweka Durtete madarakani Mwaka 2016.
"Mimi ni Mpiganaji kuanzia ulingoni na hata nje ya ulingo, nipo tayari kupigana kwa ajili ya Watu wa Ufilipino" Manny Pacquiao
Itakumbukwa Rais wa sasa wa Ufilipino Rodgrido Duterte alikubali kuwa mgombea wa Chama tawala wa nafasi ya Makamu wa Urais katika uchaguzi huo wa mwaka ujao na kama Chama chao KITAMA nikiwa am kushinda huenda Pacquiao atakuwa Rais na Durtete Makamu wa Rais.