Samirah Yusuph
Meatu.
Ongezeko la bei ya pamba kutoka tsh1050 kwa kilo hadi tsh1800 kuelekea kufikia tamati ya msimu wa  ununuzi wa pamba msimu wa 2020/2021 itahamasisha wakulima wengi zaidi kulima pamba katika msimu ujao wa kilimo.

Hayo yamezungumzwa na mkuu wa Mkoa wa Simiyu David Kafulila alipokuwa akiongea na wananchi wa kijiji cha Mwaukoli kata ya Kisesa wilaya ya Meatu mkoani humo katika mkutano wa hadhara uliolenga kutatua kero za wananchi.

Kafulila amesema kuwa bei nzuri ya pamba nchini kwa mwaka huu ni matokeo ya usimamizi mzuri wa viongozi wa serikali katika kuhakikisha wakulima wanapata  maslahi katika kilimo.

"Wanaodhani sababu ni ongezeko la bei kwenye soko la dunia pekee wanapaswa kufahamu kuwa bei ya pamba ya dola senti 90 kwa kilo iliwahi kufikiwa pia mwaka 2013 na 2018 lakini bei ya ndani imefikia tsh1800 kwa kilo".

Akizungumzia hali ya ununuzi wa pamba kwa mwaka huu katibu wa chama cha wanunuzi wa pamba nchini Boaz Ogola amesema hadi sasa jumla ya tani za pamba 133,600 zimenunuliwa kati ya makadilio yaliyokuwa tani 300,000 hadi 400,000.

Ogola amesema kutokana na makosa ambayo yamefanya kutokufikia malengo ya uzalishaji wa pamba tani 400,000 serikali imewekeza zaidi katika kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo kwa wakati.

"Sisi kama wanununuzi wa pamba ushiriki wetu unahitaji tangu awali katika kuhakikisha kila mkulima anapata mbegu bora kwa wakati pamoja na pembejeo za kilimo ili tuweze kununua pamba itayokidhi mahitaji".

Kwa upande wao wakulima wa kijiji cha Mwaukoli kata ya Kisesa wilayani Meatu
Wamekili wazi kuwa kufungwa kwa msimu wa pamba bei ikiwa juu ikilinganishwa na msimu ulivyo anza ni matumani yao kuwa msimi ujao utaanza pamba ikiwa na bei ya juu.

"Kwa bei hii inafuta machozi, lakini ili wakulima walime pamba kwa wingi serikali ilete pembejeo kwa wakati ili maandalizi yaanze mapema,"amesema Julias Jilala mkulima wa kijiji cha Mwaukoli.

Mwisho.