Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
JESHI la polisi linamshikilia Antony Lugendo (34)mkulima,mkazi wa Mlandizi kwa kosa la kumdhalilisha mtoto mdogo wa kike miaka mitatu kwa kumchezea chezea sehemu za siri.
 

Aidha limekamata watuhumiwa 38 wa makosa mbalimbali na mali za wananchi zimeokolewa,ikiwemo TV,Radio,sabufa, pikipiki na laptop.
 

Akithibitisha kutokea kwa tukio Hilo,kamanda wa polisi mkoani Pwani ,Wankyo Nyigesa ,alisema tukio limetokea juzi saa 10 jioni ,huko Kitongoji Cha Kaloleni kata ya Janga .
 

Alieleza ,mtuhumiwa alikamatwa akiwa chumbani kwake amemvua nguo zote na akiwa anamchezea mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa chekechea .
 

“Mtuhumiwa tumemkamata na upelelezi unaendelea ili hatua za kisheria zichukuliwe”alisema Wankyo.
 

Katika hatua nyingine, Wankyo alieleza kwa kipindi cha wiki mbili kuanzia septemba 3 hadi 17 septemba limefanya operesheni katika wilaya zake tano madhumuni kuzuia , kudhibiti uhalifu .
 

Katika operesheni hii walifanikiwa kukamata bunduki 1 aina ya shortgun yenye namba GP 719 na risasi moja ,bangi kwenye beg ,puli 39 ,kete 661 na miche 24,radio 2 aina ya sony na sabufa moja na spika 6 kati ya hizo aina ya boss 02 na aina ya sony nne.
 

Wankyo alifafanua ,pia laptop moja ,mafuta ya dizel lota 230 ,petrol lita 500 ,pikipiki moja aina ya boxer yenye namba za usajili MC 226 CMT rangi nyeusi na televisheni tano aina ya Good vision ,sony , Samsung,LG na TCL moja.
 

“Vitu vingine ni desktop moja aina ya dell na CPU mbili ,gari aina ya canter moja ,matairi mawili ya gari , camera mbili aina ya Samsung moja ,camera monitor,mkasi wa kukatia chuma ,funguo master key na pombe ya moshi lita 65.
 

Wankyo alikemea kwa jamii kuacha tabia ya unyanyasaji kwa watoto kwani kwa kufanya hivyo kuwaharibu kisaikolojia.