Idadi ya Watu waliofariki kutokana na tetemeko kubwa la ardhi lililotokea kusini mwa kisiwa cha Haiti imefikia 304 huku zaidi ya Watu 1,800 wakijeruhiwa ambapo hadi sasa Vikosi vya uokoaji vinaendelea na uokoaji.

Miongoni mwa waliopoteza maisha ni Seneta maarufu wa zamani, Jean Gabriel Fortune, aliyefukiwa na kifusi cha hoteli yake iliyoporomoka katika mji wa Le Cayes.


Tetemeko hilo lenye ukubwa wa 7.2 kwa vipimo vya Richter lilipiga taifa hilo masikini la caribbean asubuhi ya Jumamosi ambapo Shirika la Uchunguzi wa Miamba la Marekani (USGS) limesema idadi ya waliopoteza maisha huenda ikawa kubwa zaidi.